Mbali na Nyumbani ni riwaya ya kitawasifu inayosimulia ari ya
mhusika mkuu ya kukisaka ikipendacho roho. Ukosapo mapenzi
utaondoka nyumbani uende mbali ukayasake; ukosapo masomo
utafanya vivyo hivyo. Ukosapo mara ki au kazi utajipata barabarani
ukitamba na njia kwenda kuisaka. Je, unaposukumwa na ari au
utundu wa kitoto utaenda mbali na nyumbani kuukomesha
utundu huo na kuizima kiu ya kujua usiyoyajua? Kama ni kutafuta
maarifa, hiyo ni heri... mpaka safari igeukapo kuwa na shari ndipo
utakapobaini ukweli kwamba nyumbani hamna mfanowe hata
pawe ni pangoni.
Adam Sha katika maisha ya kiuhalisia anatoka nyumbani kwao
Zanzibar akiwa amefumwa na mkuki wa kiu ya elimu. Anapo ka
Bungoma anaselelea. Anafanya yote ya kufanywa na kijana wa
rika lake. Kisha anatumia ujanja wake kuvuka mpaka na akajipata
nchini Uganda. Anapo ka Khartoum karibu tamaa ya kuendelea
na safari inamwondokea. Kula ni kwa nadra na kulala ni taabu
tupu. Hatimaye anajipata Kairo. Anaporudi Zanzibar, nyumbani
hapamweki. Mara hii anajipata Ujerumani kwa ufadhili wa kisiasa,
ambako nako pia panamkataa. Kisa na maana?
Mbali na Nyumbani ni kisa cha matukio halisi lakini chenye msuko
wa kiriwaya na chenye sifa zote za riwaya.