Ni nani aliyetenda kitendo hiki kilichobakia kuwa siri ya kughasi, siri
iliyo sirini? Ni Kidhabi au ni Kijumwa? Hiki ni kitendo kipi ambacho
kimebaki kuwa siri iliyo chika, isiyojulikana na wazee wa mji wala vijana wa
kijiji, viongozi au waongozwa? Ni kitendo gani hiki ambacho kinaumiza
vichwa vya wafalme na vitwana, maimamu na maimuma, hadi mfalme
anapatwa na kizunguzungu kwa kupiga mbizi kilindini? Na si yeye tu,
bali lukuki ya watu! Kero inapozidi kero na siri inapozidi kusaki sirini,
mfalme anariaria na kuendelea kupiga mbizi... 'Mfalme alishtuka. Mfalme
alihangaika, mfalme alibabaika. Alipiga mbizi katika marefu na mapana ya akili
yake... Ni nani aliyefanya kitendo hiki? Kwa ajili gani? Alikifanya yeye peke
yake au kwa ushirika na wengine?
Mfalme atapiga mbizi kilindini kwenye kina kirefu na kuibuka na jibu la
kweli na ung'amuzi wa hakika?
Siri Sirini: Mpiga Mbizi Kilindini (Kitabu cha 2) ni mwendelezo wa
hadithi ya Siri Sirini: Mshairi na Mfungwa (Kitabu cha 1). Hii ni hadithi
ya kati na katika msururu wa hadithi tatu za Siri Sirini. Nayo ina
mambo matamu kuliko uki..!
Rocha M. Chimarah hakosi kuwaongoa wasomaji kwa namna alivyo
katika kusuka matukio katika riwaya ya Kiswahili. Ni mwandishi asiye
mfanowe. Anaunga ucheshi na taharuki moto mmoja na kuifanya hadithi
ya Siri Sirini: Mpiga Mbizi Kilindini (Kitabu cha 2) isiyokomeka wala kutuliwa
na yeyote anayethubutu kuisoma.
Chapa ya Longhorn Publishers

ya kati na kati katika msururu wa hadithi tatu za Siri Sirini. Nayo ina